Jerry Cornel Muro
Jerry Cornel Muro
@jerrymuro1980
 • 704
  POST
 • 288.2k
  FOLLOWERS
 • 7.5k
  FOLLOWING

Similar Instagram Profiles

Jerry Cornel Muro's Posts

Nimeona nitoe mrejesho wa wa zoezi la uandikishaji la pamoja la wananchi la kuwapatia vitambulisho vya taifa NIDA ambaoo kwa kuanzia tutatoa namba ambazo zitawasaidia wananchi wa Arumeru kuweza kusajili mitandao yao ya simu ikiwa ni kuitikia maelekezo ya Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipotoa siku 20, zoezi limekuwa na mafanikio makubwa sana na kwa sasa siku zilizobaki tunaweka nguvu katika kuwapatia namba na kuendelea kuandikisha kwa wananchi walioko pembezoni mwa kata zilizo nje ya makao makuu ya wilaya kwa Halmashauri zote mbili Meru na Arusha Dc #Arumeru_Yetu #WananchiWetu #NidaYetu #Mwaka2020MatendoZaidi
Fanya mambo ya msingi, kisha tembea kwa rahaa #Arumeru_Yetu #FamilyKwanza
Leo nimepata nafasi ya kumjulia hali mama yangu mzazi Bi. Ankunda Muro ambae amelazwa kkt taasisi ya magonjwa ya moyo jakaya kikwete hapa hospitali kuu ya muhimbili , nimefarijika kuona matibabu na vipimo ambavyo angetakiwa kufanyiwa nje ya nchi sasa vinapatikana nchini kwa kiwango kizuri na cha kuridhisha sana, matibabu ya magonjwa ya moyo ni ghali sana lakini kwa kuwa serikali imeweka mfumo wa utoaji wa matibabu kwa njia ya bima ya afya kupitia NHIF hakika nimeamini kuwa sasa hakuna mwananchi ambae anaweza kupoteza maisha kwa kukosa huduma bora za afya na kwa gharama nafuu, mimi na familia yetu tumeona kwa macho, niseme jambo kwa wanatanzania wenzangu ili tuweze kumudu gharama za matibabu lazima ifike mahali tubadili mtazamo wetu na kuanza kuyapa kipaumbele mambo yenye thamani katika maisha yetu ikiwemo kujiunga na mfuko wa biama ya afya Kupitia NHIF ambao wameboresha huduma za bima zenye gharama nafuu mpaka vijijini, najivunia kupata fursa ya kumsaidia kazi Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli nimeona dhamira yake, matendo yake na utashi binafsi wa kisiasa wa kuifanya Tanzania nchi bora ya kuishi #GetwellSoonMumy♥️♥️♥️ #AfyaYetu #HakunaKamaMama
It’s not what we have in life, but who we have in our life that matters #MabintiWaNguvu 💪🏾💪🏾 #AlwaysProudofYouTwins♥️♥️
Nimeona ni busara kufanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya mifugo ya wananchi wetu haswa wa jamii ya kifugaji Halmashauri ya Arusha, nimetembelea na kukagua mabwawa mawili katika kijiji cha Engutukoiti kata ya oldonyowasi sisi kwetu tunajiandaa kabla ya kiangazi, uongozi ni kujipanga ma kuona mbali na kujiandaa na yajayo #2020Kazikwetu #WafugajiWetu #ArumeruYetu
Msingi wa Serikali ni wananchi na sisi tunawasikiliza wananchi wetu tunatatua kero na changamoto zao kwa haraka na wakati muafaka, tunaamini jamii inataka kusikilizwa na kutatuliwa changamoto wanazokutanazo katika maisha yao ya Kila siku, #2020MatendoZaidi #ArumeruYetu #WananchiWetu #SerikaliYao
Nimewasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya wilaya ya kichama ya Meru, kwetu ilani imetekelezwa kwa wastani wa zaidi ya asilimia 90% ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 43 tangu kuasisiwa kwa cha mapinduzi CCM #2020MatendoZaidi #ArumeruYetu #chamachetu
Alichokisema Profesa Patrick Lumumba baada ya kumaliza mazungumzo na Mhe Rais, Dkt. John Magufuli, pia waweza tazama full clip instagram @jerrymuro1980
Naomba kuweka kumbukumbuk sawa, katika mahojiano yangu nilisema na nanukuu ‘’ kwa sasa haji manara akatafute kazi ingine nzuri ambayo ataifanya baada ya kufikia ukome wa maisha yake kwenye soka, na nikakushauri kazi itakayokufaa ni kwenda kuwa mwalimu wa madrasa ‘’ sasa tatizo liko wapi hapo? Kwani wewe hujasoma vizuri Quran takatifu mpaka ushindwe kufundisha wengine? Kwani wewe huwezi kuwa mwalimu wa madrasa? Au kwa kuwa unakaa na unazungukwa na hao wanaokutia ujinga? Sikiliza kijana katika hili pambana na hali yako na usingize mwamvuli wa dini katika michezo, kama kosa langu ni kukushauri ukawe mwalimu wa madrasa jambo ambalo nimekushauri vizuri na nimekushauri jambo jema basi niwie radhi, mwisho uache tabia ya kutafuta kichaka cha kujificha unapokuwa unashikwa vizuri!! Nadhani unanijua nikiamua kukushughulikia katika mpira kamwe huwa sikoseagi najua nakupigia wapi za chembe mpaka unakaa chini na maji unaita mma!! Hiyo ilikuwa ni trelaa picha lenyewe linakuwaja tarehe 08/03/2020 pale Taifa kaa vizuri kazi imeanza sasa, mwisho kumbuka nilipokutoa wewe kijana na uwe na adabu na wakubwa zako💪🏾💪🏾💪🏾@hajismanara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli tarehe 28 Februari, 2020 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti mkubwa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Msikiti huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco baada ya kuombwa na Rais Magufuli alipofanya ziara rasmi hapa nchini Oktoba 2016.
Akiongozwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally, Mhe. Rais Magufuli amejionea kazi za ukamilishaji wa jengo jipya la Msikiti na jengo la ofisi ya Taasisi ya Mfalme Mohammed VI wa Morocco zikiendelea kukamilishwa, na ameelezea kufurahishwa kwake na ubora na uzuri wa Msikiti huo.
Rais Magufuli amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa kutekeleza ombi alilomuomba la kuwajengea Waislamu Msikiti mkubwa kuliko yote hapa nchini, na amempongeza Mufti wa Tanzania na Waislamu wote kwa kujengewa nyumba nzuri ya Ibada.
Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally amemshukuru, Rais Magufuli kwa kuwajali Waislamu na kuwaombea msaada wa kujengewa Msikiti huo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 97.

Akiwa na viongozi wenzake wa BAKWATA, Sheikh Mkuu Aboubakar Zubeir bin Ally ameongoza Dua ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli na kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aiepushe Tanzania dhidi ya maradhi ya homa ya virusi vya corona, kudumisha amani na utulivu na kuombea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu ufanyike vizuri na kwa amani.
‘’Mimi ni Askari niliyeiva huwa sitingishiki hata kwa upepo wa aina gani..! Na mara nyingi waliojaribu kunitingisha, walitingishika wenyewe! Hawa watu walipojaribu kutingisha kwenye masuala ya kiuchumi, walitingishika wenyewe!” - Rais, Dkt. John Magufuli #SisiNiTanzaniaMpyA+
Mwaka huu utarejesha kila kitu, sasa rejesha na cheti cha watu cha kill marathon, mwaka wa tabuu huu @hajismanara halafu @albertomsando msaidie kujua sheria inasemaje ya urejeshaji wa vitu vya watu 🚶🏽‍♂️🚶🏽‍♂️🚶🏽‍♂️🚶🏽‍♂️shubamitttttt kwa hisani ya @officialmwalubadu