Mwanamke Thamani
Mwanamke Thamani
@mwanamkethamani
 • 309
  Post
 • 1.3k
  Followers
 • 7
  Following

Mwanamke Thamani's Posts

MAANA YA17 ZA IMANI

Maana ya 7

Imani ni nguvu ya kiroho inayokuja baada ya kupata mguso wa Neno unaopelekea binadamu kutenda ishara, miujiza na maajabu na kuhesabiwa ana haki mbele za Mungu

Wagalatia 3:5-6
MAANA 17 ZA IMANI

Maana ya 8

Imani ni uwezo wa kujiona kama vile Mungu anavyokuona kwenye Neno lake

Ni lazima uweze kujiona kwenye Neno la Mungu kwanza kabla ya kufanyika kuwa hilo, Yohana Mbatizaji alijiona kama
.
. 
Yoh 1:23
MAANA YA 17 ZA IMANI

Maana ya 9

Imani ni mfumo wa kuishi ambao unamwezesha kila mwamini kuweza kushinda majaribu, vishawishi pamoja na matatizo yote ya duniani

Binadamu ameumbwa aishi kwa imani na siyo kwa kile anachokiona kwa macho ya nyama 
Hab 2:4 Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake
MAANA 17 ZA IMANI

maana ya 10

Imani ni uchaguzi, uamuzi na kusudio ambalo ni lazima mwamini alifanye kama anataka kuishi maisha ya furaha katika sayari hii

Yoshua 24:15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.

Ni dhahiri hakuna ambaye anapokea kitu kama hajaamua kuamini atakipokea, unaamua kumtumikia Mungu peke yako baada ya kuamini kwamba ahadi za Neno lake ni kweli na hakika

Imani siyo hisia, kwa sababu hisia siyo kitu cha wakati wote na imani inapaswa kuwepo muda wote ili iweze kuzaa matokea yanayohitajika 
Hatuwezi kuwa watendaji sahihi wa kazi za Mungu pasipo imani, tunaweza tuu kuona udhihirisho wa nguvu zake kwa imani, na udhihirisho huu siyo wa hisia ni halisi 
Lakini kuweza kuamini Neno la Mungu na kujengeka kwa imani yetu siyo kazi yetu pekee bali tunawezeshwa na Roho Mtakatifu 
Zach 4:6
Bwana Yesu Kristo asifiwe, asubuhi saa tatu na nusu hakikisha unafungua radio yako ya PRAISE POWER 99:3 FM 
Nitakuwa hewani nikifundisha Neno la Mungu mubashara kutokea studio za Praise Power ambalo litakufungua katika hali unayopitia katika Jina la Yesu Kristo
MAANA 17 ZA IMANI

Maana ya 10

Imani ni uchaguzi, uamuzi na kusudio ambalo ni lazima mwamini alifanye kama anataka kuishi maisha ya furaha katika sayari hii

Yoshua 24:15
MAANA 17 ZA IMANI

Maana ya 11

Imani ni tumaini la injili linalopatikana katika kuhudumu 
Wakolosai 1:23
MAANA 17 ZA IMANI

Maana ya 12

Imani ni njia ya kumwendea Mungu ili tuweze kumkumbusha haki zetu, inayoondoa kutahayarika maishani mwa kila aaminiye.

Rom 9:32
MAANA 17 ZA IMANI

Maana ya 13

Imani ni kiapo cha kiroho cha kutokuacha wala kutokuangalia pembeni wakati unahitaji kitu na hata baada ya kukipata, ni kung'ang'ania mpaka unachokihitaji na kuendelea

Hatumwamini Mungu tuu kwa sababu anaweza kutupatia kile tunachihitaji, La hasha bali ni kwa sababu tunampenda, na tunapaswa pia kufahamu imani yenye nguvu ni inayochochewa na upendo

Katika siri ya Imani kinachomfanya muamini aendelee kubakia kwa Mungu hata baada ya kupata baraka za kila namna ni upendo, Imani ambayo haina msingi kwa upendo na Mungu humomonyoka mawimbi yanapokuja 
Wagalatia 5:6
MAANA 17 ZA IMANI

Maana ya 14

Heb 11:1
MAANA 17 ZA IMANI

maana ya 15

Imani ni kuolewa na Mungu ili kuweza kushirikiana naye kutimiza kusudi fulani, Kut 19:5
MAANA 17 ZA IMANI

Maana ya 16

Imani ni mfumo wa mawasiliano baina ya mtu na Mungu ambao unafuata utaratibu maalumu ili kuweza kuleta matokeo kwa anayeutumia

Mfumo ni mjumuiko wa vitu vinavyofanya kazi kwa pamoja huku vimeunganika ili kukamilisha suala moja, imani siyo nguvu inayotenda kazi peke yake inaambatana na matumaini 
War 4:18
KUNA MTU AMESHIKA UFUNGUO WAKO!

Wote tunamuomba sana Mwenyezi Mungu atubariki na atupe hili na lile lakini ukweli ni kwamba Mungu hajawahi kutuletea fedha hata siku moja bali humtumia mtu fulani kutubariki

Mungu anakupatia kitu au kukubariki kupitia mtu fulani ambaye anamleta katika maisha yako, hivyo baraka zetu Mungu anaziachia kupitia mtu fulani ambaye atamuagiza aje afanye kitu fulani ambacho ndio kitakupa mpenyo wa kwenye suala linalokutatiza

Hii ndio sababu tunapaswa kuishi kwa kupendana na kujaliana sisi kwa sisi sababu funguo za maisha yako ziko kwa Mungu na Mungu ni pendo ni lazima tupendane ili aweze kuachilia funguo wako kupitia mtu fulani au kukupa maarifa na ufunuo wa kukufanikisha

Katika kijiji kimoja kulikuwa na vita baada ya jeshi moja kushinda wakawateka wenzao na kiwapeleka porini ambapo kulikuwa na kambi ya mateka wa vita

Katika kijiji hicho kulikuwa na matajiri kadhaa wanaopenda kuona watu wakipata majitaji muhimu na wakiishi vyema/watoa misaada (philanthropist ) baada ya matajiri hawa kupata taarifa wa kwanza akaenda kwa mkuu wa watekaji akamuambia.... Najua mmewateka mateka hawa kwenye hii kambi hakuna maji na umeme ninaomba mniruhusu nijenge miundo mbinu ya maji safi na salama na umeme ili wasiteseke, tajiri huyu akaruhusiwa akatimiza haja yake na akaufurahisha moyo wake

Tajiri wa pili naye akaja na haja ya kuwajengea na kiwatengenezea vitanda na sehemu nzuri za kupumzika basi mkuu wa kambi akamruhusu huyu naye akaridhika kwamba haja ya moyo wake imeshatimia

Tajiri wa tatu akasema yeye ana mashamba mengi na analima sana ataleta vyakula vya aina tofauti kwa sababu chakula walichokuwa wanakula pale hakiridhishi na kilikuwa duni, huyu naye akaruhusiwa akatimiza haja yake na kufurahia sana kuona mateka wale kila siku wanakula vyema

Tajiri wa nne ambaye alikuwa hafikiri kama wenzie, alifikiria zaidi akachunguza na kufahamu sehemu ambayo wanaweka ufunguo wa kambi ile basi baada ya kufahamu usiku wakiwa wamelala akaenda kuiba funguo zile akawafungulia mateka wale wakaondoka

Neno la Mungu limetofautisha uhuru, kuna uhuru unaweza kuupata kutokana na mtu kukusaidia jambo fulani katika hali ya kibinadamu, lakini kuna uhuru utokao juu huu
Tuwe pamoja Asubuhi hii Praise Power Radio kwenye kipindi cha Mwanamke na Huduma kuanzia saa tatu na nusu mpaka saa nne kamili

Hakikisha unafungua redio yako kusikiliza kipindi hiki kitakubariki na kukufungua katika Jina la Yesu Kristo
BARTIMAYO ALIZINGATIA HAYA

Hakuna kisingizio chochote unachoweza kutumia kama haujafikia lengo lako katika maisha ila ukweli ni kuwa haujawa na shauku na kiu ya kutosha

Wengi wanataka uponyaji, muujiza, mafanikio na mipenyo kwenye maisha lakini kiu na shauku yao ya kutaka vitu hivi haijatosha, na haijamshitua Mungu hata aweze kuwapatia

Zaburi 63:1
KUOMBEA WATOTO WETU NA FAMILIA KWA UJUMLA.

Andiko kuu:
Luka 23:28
IMANI NI FEDHA YA KIROHO

Neno la Mungu ni pana sana, huwezi kulielewa kwa akili yako binafsi ndio maana tunahitaji nguvu za Roho Mtakatifu ziweze kutufunulia kile ambacho Mungu ananena nasi katika Neno lake ili tuweze kukielewa vyema na kukifanyia kazi kama inavyotupasa

Tunapaswa kutambua kwamba siri za Mungu hufunuliwa na Roho kwa wale ambao anawapenda nao ni wale wanaolishika Neno la Mungu 
1Kor 2:10
Bwana Yesu asifiwe! Kwa wale mnaonipigia simu na kuniandikia sms naomba niweke wazi hapa hii siyo account halisi ya Mwanamke Thamani

Account yetu ina Logo ya Mwanamke Thamani na hatuwaoneshi watu fursa wala kufanya network marketing
.
.
Tafadhali sana usije ukajihusisha na account hii niliyoiscreenshot ukidhani unawasiliana na Management ya Mwanamke Thamani
.
.
Account halisi ni @mwanamkethamani na siyo hii fake ya @mwanamke_thamani
.
.
Mungu akubariki sambaza na kwa wengine kwa utukufu wa Bwana
MAANA 17 ZA IMANI--SEHEMU YA PILI

Tunaendelea na somo letu jana tuliona maana ya kwanza ya imani na leo tutaendelea na maana ya pili ya imani kulingana na Neno la Mungu

IMANI ni uwezo wa kupandwa ndani ya Kristo naye ndani yako ili uweze kuzaa matunda 
Yohana 15:4
Zanzibar mpo tayari? 
Mwisho wa mwezi wa kumi na moja tunakuja kumtangaza Kristo kwa nguvu na ushujaa mwingi huko, pangilia mambo yako mapema

Hakikisha hii siku unaitenga kwa ajili ya Yesu Kristo, kwa maelekezo zaidi tafadhali wasiliana na kamati ya maandalizi kwa simu zifuatazo

0712 262 801
0776 644 665
MAANA 17 ZA IMANI

Leo tunaangalia maana ya tatu

IMANI ni ule uwezo wa kuweka pembeni hekima ya kidunia na ya kibinadamu, uzoefu na ushawishi ili uweze kumruhusu Roho Mtakatifu kukutumia kama chombo kitakacholeta matokeo yanayohitajika 1Kor 2:1-5

Watu wengi wanaamini katika elimu zao, uzoefu wao, watu wanaowafahamu nk lakini hii ni kinyume na Neno la Mungu unapaswa kuwa navyo hivyo lakini imani yako haipaswi kuwa katika hivyo kwa sababu havikupatii nguvu ya kutenda kazi bali Mungu Wafilipi 4:13
Tuwe pamoja asubuhi hii Praise Power Radio kuanzia saa tatu na nusu mpaka saa nne asubuhi hii kwenye kipindi cha Mwanamke na huduma

Leo tutaendelea na somo tuliloanza kipindi kilichopita la Kipofu Bartimayo kiundani, hakikisha unafungua radio yako Dar ni 99:3 FM
MAANA 17 ZA IMANI

Maana ya Nne! 
Imani ni uwezo wa kufanya kila kitu kulingana na Neno la Mungu

Zaburi 119:105
MAANA 17 ZA IMANI

Maana ya 5

Imani ni uwezo wa kugusa nguvu za Mungu, kujiungamanisha na shuhuda za wengine na kuweza kuutambua mkono wa Mungu kwenye maisha ya wengine na kuutumia kama fursa ya kubadili maisha yako 
Imetoka Mdo 16:25-34

Kumbuka hakuna imani inayozaliwa pasipo kuwa na ufahamu, pale tunapolijua neno la Mungu inatusaidia sana kuchochea imani yetu, Paulo na Sila walitambua kwamba wanapaswa kumsifu Mungu ili waweze kuuona ukuu wake 
Isaya 43:21